Episodesammendrag
Kwa miaka mingi, adhabu ya viboko imekuwa mojawapo ya njia zinazotumiwa na walimu kudhibiti nidhamu ya wanafunzi shuleni nchini Tanzania. Hata hivyo, matumizi yake yameendelea kuzua mjadala kutokana na madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa watoto. Novemba 3, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi wa kihistoria wa kubatilisha vifungu vya kanuni zilizokuwa zikiruhusu adhabu ya viboko mashuleni, jambo lililo ibua mjadala nchini humo. Tunaangazia na kujiuliza Je, Tanzania iko tayari kujenga mfumo wa nidhamu usiotegemea nguvu za kimwili? Huku baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki zikifuta kitambo adhabu hiyo

Episoder
Kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni nchini Tanzania
Lyttet tilKwa miaka mingi, adhabu ya viboko imekuwa mojawapo ya njia zinazotumiwa na walimu kudhibiti nidhamu ya wanafunzi shuleni nchini Tanzania. Hata hivyo, matumizi yake yameendelea kuzua mjadala kutokana na madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa watoto. Novemba 3, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi wa kihistoria wa kubatilisha vifungu vya kanuni zilizokuwa zikiruhusu adhabu ya viboko mashuleni, jambo lililo ibua mjadala nchini humo. Tunaangazia na kujiuliza Je, Tanzania iko tayari kujenga mfumo wa nidhamu usiotegemea nguvu za kimwili? Huku baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki zikifuta kitambo adhabu hiyo
Makala: Hali ya usalama Beni, uwezo wa ADF na changamoto za serikali ya DRC
Lyttet tilMauaji ya raia, mashambulizi dhidi ya vijiji, utekaji nyara na uharibifu wa mali vimeendelea kuibua maswali kuhusu uwezo wa serikali ya DRC kuwalinda wananchi wake. Katika Makala ya Afrika Mashariki, hii leo tunaangazia nyuma ya mauaji ya ADF, nani anaendeleza vurugu mashariki mwa DRC?
Mauaji katika ndoa na migogoro ya kimahusiano Afrika Mashariki
Lyttet tilHii leo tunaangazia mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, tukichunguza takwimu zilizopo, na sababu zinazochangia ukatili huo.
Teknolojia ya anga na matumaini mapya kwa jamii za bonde la Ziwa Victoria
Lyttet tilKatika mwambao wa Ziwa Victoria, mamilioni ya wananchi wanategemea kilimo, uvuvi na ufugaji wa samaki kwa ajili ya chakula na kipato. Hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi, kutotabirika kwa hali ya hewa na changamoto za uzalishaji vinaendelea kuathiri maisha yao. Je, teknolojia za satelaiti zinaweza kumsaidia mkulima kujua wakati unaofaa kupanda, mvuvi kufanya maamuzi sahihi na mfugaji wa samaki kupunguza hasara? Kupitia mradi wa KijaniSpace unaotekelezwa Tanzania, Kenya na Uganda kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya, teknolojia za anga na taarifa za kidijitali zinatazamwa kama sehemu ya suluhisho la changamoto hizo. Karibu katika Makala ya Afrika Mashariki, hii leo tunaangazia namna ubunifu wa kiteknolojia unavyoweza kubadili maisha ya wananchi wanaoishi katika bonde la Ziwa Victoria.
Urembo kwa njia ya upasuaji
Lyttet tilKaribu katika makala ya Afrika mashariki inayochunguza uhusiano kati ya urembo, kujiamini na shinikizo la kijamii. Tutaangazia simulizi za mwanawake aliyechagua kufanyiwa upasuaji wa urembo, pamoja na mitazamo ya wataalamu na wananchi.